Friday, April 7, 2017

Utoaji mimba( abortion)





 







Mimba kutoka ni tokeo la mambo tofautitofauti, kama matumizi ya kemikali au kwa mjamzito  ambazo zina kemikali zinazosababisha mimba kutoka endapo zitatumiwa bila maelezo sahihi kutoka kwa mtaalamu wa afya, Dawa nyingi zinazotibu magonjwa mbalimbali zinaonyesha wazi kwamba mwanamke mjamzito anaruhusiwa ama la, na hata akiruhusiwa zinaeleza kwamba atumie chini ya uangalizi wa mtaalamu wa afya.
Lakini Kutoa mimba kwa kusudia endapo mwanamke hana utayari wa kulea mimba au hajajiandaa kupata mtoto kwa wakati huo ni Moja ya vitu ambavyo Wanawake wengi wanajihusisha navyo, napengine kuhofia namna ambavyo jamii itawatazama hufanya mambo haya kwa kujificha sana hii huwafanya wengi kutoa mimba kiholela na kuhatarisha maisha yao.

Hatua za utoaji Mimba
Mimba changa ambayo tayari ipo kwenye mji wa mimba hutolewa kwa kutumia kemikali zilizo kwenye madawa,au vifaa maalum vinapitishwa njia ya uzazi wa mwanamke mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kuanza kutoa kitoto ndani ya mji wa uzazi.

Njia salama  ya utoaji mimba huwahusisha wataalamu wa afya ya uzazi na njia za kiholela mtoaji mimba hutumia njia zisizo rasmi na kuharibu mimba.

Uhalali wa Utoaji Mimba
Sheria za dini kama dini ya kikristo hairuhusu utoaji mimba.
Kuna baadhi ya sheria za nchi Kama Tanzania ambazo haziruhusu kabisa utoaji wa mimba lakini katika nchi zilizo endelea kama marekani sheria zinaruhusu utoaji mimba salama.

Madhara ya utoaji mimba 
Ni kama vifo,ugumba na utasa kwa mwanamke,pia mwanamke anaweza kuathirika kisaikolojia kutokana na mawazo ya kuharibu nakuuwa kiumbe kisichokuwa na hatia.

Epuka ngono zembe, tumia njia za uzazi wa mpango, epuka kufanya mapenzi kabla ya ndoa kuepuka utoaji haramu wa mimba.
Tafuta washauri wa afya pale utakapo gundua kuwa na mimba ili upate ushauri thabiti wa nini cha kufanya.

 Picha zifuatazo zinaonyesha viumbe au mimba changa zilizokatishwa maisha na haki ya kuishi.







MAONI YA MWANDISHI 
Wakati wewe unatoa mimba kuna watu wanahangaika kutafuta watoto, wanavunja mahusiano ama ndoa kwa kukosa watoto, wanakesha wakiomba kutafuta watoto, kama umepata ujauzito bila kupanga ni bora ukazaa na ukatafuta watu wenye uhitaji na kuwa adopt watoto kuliko kuua.

Hakuna haja yakupata ujauzito kama huwezi kuikuza mimba tumia njia za uzazi wa mpango ili ujiepushe kuua kiumbe kisicho na hatia kwa starehe zako binafsi.


MAGONJWA YA NGONO

 Muandishi, Dr. Gaudence Mathew


Magonjwa ya ngono ni kundi la magonjwa ambayo huenezwa kwa njia ya kujamiana/kukutana kimwili/kufanya tendo la ndoa.
Kuna aina nyingi za magonjwa ya ngono na yamegawanyika katika makundi kulingana na dalili na alama yanazosababisha
MAGONJWA YANAYOSABABISHA KUTOKWA NA UCHAFU/USAHA SEHEMU ZA SIRI

– KISONONO (GONORRHEA)
– KLAMADIA (CHYLAMADIA)JAMII YA KISONONO
– FANGASI (GENITAL CANDIDIASIS)
– TRAKOMONIASISI (TRACOMONIASIS)
– KISAMAKI 

 DALILI ZAMAGONJWA YANAYOSABABISHA KUTOKWA UCHAFU/USAHA SEHEMU ZA SIRI

• Kutokwa uchafu/usaha sehemu za siri.
• Maumivu makali ya tumbo lote(wanawake).
• Kuwashwa sehemu za siri
• Maumivu chini ya kitovu (wanawake)
• Maumivu wakati wa kujamiana
• Maumivu makali wakati wa kukojoa(hasa wanaume)

MADHARA YA MAGONJWA YANAYOSABABISHA KUTOKWA UCHAFU/USAHA SEHEMU ZA SIRI
Kwa wanawake:-

Uke Ulioathirika

• Uambukizo kwenye pango la nyonga(PID)
• Ugumba/utasa.(INFERTILITY)
• Mimba kutunga nje ya tumbo la uzazi.(ECTOPIC PREGNANCY)
• Maumivu makali ya tumbo(PERITONITIS)
Kwa wanaume.
• Kuziba mkojo,(URETHRAL STRICTRES)
• Kuvimba mapumbu(ORCHITIS)
• Utasa. (INFERTILITY)

Kwa watoto wachanga:-Kutokwa usaha kwenye macho na Upofu

Mtoto alie athirika na Ugonjwa wa Ngono akiwa Tumboni