-->
mlokamili wenye virutubisho vyote ukizingatiwa unasaidia
kuepukana na magonjwa kama saratani, kisukari, magonjwa ya moyo na
magonjwa ya mifupa.
Zingatia yafuatayo.
PATA KIFUNGUA KINYWA KIZURI
Wahenga wanashauri kwamba pata kifungua kinywa chenye hadhi ya
kifalme,chakula cha mchana (lunch) kama mtoto wa mfalme na chakula
cha usiku (dinner) kama mtumwa, ukipata kifungua kinywa cha nguvu
asubuhi itakusaidia kufanya kazi zako wa umakini zaidi na pia
itasaidia kubudget pesa yako kwani hutakuwa na ulazima wakununua vitu
vidogodogo vya kula.
Pata milo mitatu kwa siku kila siku
Nimuhimu kuzingatia hili kwani kwakufanya hivi utakuwa ni mwenye
nguvu sikunzima,hivyo kuepuka matatizo ya tumbo hasa vidonda vya
tumbo.
Pika chakula wewe mwenyewe kuliko kununua
Nunua viungo mbalimbali vitavyokusaidia wakati wakujitayarishia
chakula,kujipikia kunapunguza gharama na pia ni nafuu, pia
itakusaidia kupika chakula katika kiwango unachotaka,kama vile kiasi
cha chumvi, kwani ni nzuri zaidi chumvi ikiivia jikoni kuliko
ikiongezewa wakati wa chakula, vilevile inasaidia kufanya mabo yako
kwa usafi zaidi kwakuwa mtu yeyote mwenye akili timamu atajali afya
yake.
Chakula cha usiku.
Nivizuri kupata chakula chepesi ili kusaidia mmengenyo wa chakula
usiku ukiwa umelala kasi ya mmeng'enyo hupungua tunapokuwa tumelala.
Kula matunda kwa wingi
Nivizuri kula matunda kwa wingi itakusaidia kuongeza vitamins, na
kuukinga mwili na magonjwa.
Kunya maji mengiItakusaidia katika mmeng'enyo wa chakula,kusafisha tumbo pamoja nakusaidia utoaji taka mwilini
No comments:
Post a Comment