Monday, July 16, 2012

Mlo kamili(Balance diet)


-->

mlokamili wenye virutubisho vyote ukizingatiwa unasaidia kuepukana na magonjwa kama saratani, kisukari, magonjwa ya moyo na magonjwa ya mifupa.
Zingatia yafuatayo.

PATA KIFUNGUA KINYWA KIZURI

Wahenga wanashauri kwamba pata kifungua kinywa chenye hadhi ya kifalme,chakula cha mchana (lunch) kama mtoto wa mfalme na chakula cha usiku (dinner) kama mtumwa, ukipata kifungua kinywa cha nguvu asubuhi itakusaidia kufanya kazi zako wa umakini zaidi na pia itasaidia kubudget pesa yako kwani hutakuwa na ulazima wakununua vitu vidogodogo vya kula.

Pata milo mitatu kwa siku kila siku

Nimuhimu kuzingatia hili kwani kwakufanya hivi utakuwa ni mwenye nguvu sikunzima,hivyo kuepuka matatizo ya tumbo hasa vidonda vya tumbo.



Pika chakula wewe mwenyewe kuliko kununua

Nunua viungo mbalimbali vitavyokusaidia wakati wakujitayarishia chakula,kujipikia kunapunguza gharama na pia ni nafuu, pia itakusaidia kupika chakula katika kiwango unachotaka,kama vile kiasi cha chumvi, kwani ni nzuri zaidi chumvi ikiivia jikoni kuliko ikiongezewa wakati wa chakula, vilevile inasaidia kufanya mabo yako kwa usafi zaidi kwakuwa mtu yeyote mwenye akili timamu atajali afya yake.

Chakula cha usiku.

Nivizuri kupata chakula chepesi ili kusaidia mmengenyo wa chakula usiku ukiwa umelala kasi ya mmeng'enyo hupungua tunapokuwa tumelala.

Kula matunda kwa wingi

 


Nivizuri kula matunda kwa wingi itakusaidia kuongeza vitamins, na kuukinga mwili na magonjwa.

Kunya maji mengiItakusaidia katika mmeng'enyo wa chakula,kusafisha tumbo pamoja nakusaidia utoaji taka mwilini







Thursday, July 12, 2012

Matumizi ya asali katika tasnia ya urembo (the use of honey in the beauty industry)
                Asali inatibu chunusi (honey treats acne)


Mazao asilia ya mimea na matunda vilevile mazao yanayotoka kwa wanyama ni njia salama zaidi ya kutibu chunusi.lakini pia asali ni njia nzuri ya kutibu chunusi, kuondoa mabaka na kufa

nya ngozi yako iwe laini.


Mchanganyiko wa asali na mdalasini yanaweza kutumika kutibu chunusi

Hapa ni jinsi ya kutumia asali na mdalasini kutibu chunusi: Chunusi ni tatizo linalowasumbua watu wa umri mbalimbali, vijana kwa watu wazima na jinsia zote, matumizi

Asali kijiko kimoja, unga wa mdalasini kijiko kimoja, changanya vizuri kisha upake eneo lililo athirika safisha uso na maji ya uvuguvugu baada ya dakika ishirini.




Tafadhali kumbuka
fanya  hivyo mwenyewe. Kama utasikia ngozi kuwasha tafadhali acha kutumia.Dawa hii inaweza kufanya kazi kwa kila mtu. Tiba hii hufanya kazi  kwa aina mbalimbali ya ngozi.


Unaweza pia ukalala na kipako ulichopaka yaani mchanganyiko uliouandaa baada yakukauka kisha asubuhi ukaosha uso kwa maji ya uvuguvugu.